TOPBAND

TOPBAND

Thursday, May 27, 2010

KIWANJA KIPYA.

LEO MASAI CLUB PANACHIMBIKA!

HAYA wapenzi wa sanaa za live band muda umefika leo ndo leo hapo MASAI CLUB MBNA patamu sana mziki mzima wa TOPBAND utawasha moto mkubwa chini ya MKALI WAO T.I.D karibu ujimix na mastaa wakweli

JAFFARAI VIDEO SHOOT!

IT looks crazy am puttin this image i wonder if we could get a chick with a same smile n character like her in our video shoot which will take place in bagamoyo on saturday mhh lets wait tuone may be we shud send a ticket kwa miss JULLIANA wat a SMILE!

Saturday, May 8, 2010

HASHIM THABEET AMENIPiGA.

Ilikua majira ya saa kumi unusu nikiwa natoka club billcanas pamoja na rafiki yangu ANNA tukiongozana kuelekea mlango mkubwa wa kioo nikiwa naongea na simu na Hisbert kwa sauti ya juu maana kelele za muziki zilikua zinasumbua nikiwa nimesimama nje ya mlango wa kioo ghafla akatokea bwana HASHIM ambaye alikua counter akiongea na wakata ticket akaja nje na kunipiga bonge la mtama nikaaunga chini ya sakafu na kuzirai kwa dakika kadhaa,mabaunsa wakanibeba na kuniweka pembeni maana nilikua mlangoni,nilipozinduka nilisikia maumivu makali kwenye mabega,mkono wangu wa kulia na mguu ambao unafanya kutembea kwangu kwa taabu,nikaangalia mkononi simu yangu sikuiona tena,nikawauliza mabaunsa wake jamaa amekwenda wapi!wakadai ameondoka tayari...nikajikokota kuelekea kwenye gari yangu na kuelekea polisi kutoa taarifa niweze kupata matibabu,nilipofika nikaaandika statement nikapewa namba ya case CD/RB/6848/10 pia nikapatiwa PF3 nikaenda hospitali nikapata matibabu,sasa hivi niko kitandani siwezi kutembea vizuri,pia nitashindwa kuperfom kwenye harusi ambayo tayari nishalipwa pesa tayari.SWALI langu ni kwanini ameamua kunidhalilisha vile mbele ya CLUB na FANZ ambao nilikua nawatumbuiza?kwanini ameamua kuniharibia kazi yangu?kwanini ameamua kunipiga bila ya kumkosea?JE NI SAWA HIVI JAMANI....naona  MACHOZI YANANITOKA SINA CHA KUMUELEZA MAMA YANGU.