TOPBAND

TOPBAND

Tuesday, March 30, 2010

SIWEZI KUSHIRIKI!

Naomba radhi kwa mashabiki wangu wote kutoka pande zote za sayari hii najua mlikua mnasubiria kunipigia kura kwenye hiki kinyanganyiro cha award hizi za kilimanjaro,najua imekua uamuzi muafaka kwangu kujitoa kwene awards hizi basi naomba muelewe sababu zangu hizi za msingi:
1.Kwanza nahisi mimi kama TID na mziki ninao perfom kwa kipindi chote hiki cha miaka saba toka nimepewa tunzo hizi sina umuhimu wa kuwa shiriki sababu hata nikitengeza wimbo ambao unakubalika sana na wapenzi wa muziki huu wa kizazi kipya sipewi tuzo kwa mantiki hiyo naona sioni sababu ya kuwa kwenye tuzo hizi.
2.Pia nilidhani labda ni upungufu wa mawazo ya majaji ama waandaaji ambao imewezekana nilitofautiana nao kipindi fulani nilipokuwa nafanya nao kazi za maonesho,inauma sana unapoona wengine ambao uko nao kwene same field wanapewa nafasi kubwa ambayo pia mimi nastahili kutokana na juhudi ambazo nafanya kwenye sanaa hii ya kizazi kipya hapa nahisi sihitajiki kwani kama wimbo wangu wa bendi ni bora wa mwaka kwanini nisiwe mwanamuziki bora wa kiume mwaka huo,pia hata video zangu huwa za viwango vya juu nazo hazipewi nafasi kwenye video bora za mwaka!
3.Kwa sababu hizi ambazo mimi naona kwangu hazinijengi sioni sababu ya kuwepo kwenye TUNZO hizi tena kwani sidhani kama ni wakati wa kuwaangusha mashabiki wangu ambao natumia muda mwingi na effort binafsi bila ya mdhamini kuwaunganisha na muziki wangu basi nisameheni kama nimewakosea lakini hainisaidii chochote endeleeni na hao mnaowapa kila category i will never stop making good music for my country surely i wont,i was born to do THIS,..  THANKS.
1.

Monday, March 29, 2010

NIKOMESHEE MANAGER!

Hapa namwona manager dacota akihema kwa kimwana ngwasuma jamani  mbona HAZIKABI ENTERTAIMENT!

QUICK SNAP!

Yea i had to rush for a quick snap coz tha stage was waiting for me oh god could hear tha songlak playing  sikuacha kupiga picha na huyu BINTI yea jana was soooooooooooo fun!

KAZI GANI!!!??

Huyu mrembo alikuwa ndo anaingia ndani mhh kamera yetu iliposhindwa kujizuia heee she iz hot hebu mcheki alivopendeza wow na hako ka beauty spot.......

HIZI BATA JAMANI!

From far left NI TOP,NACHA,NUNUU,KIM AND FATMA.....haikua bata ya kitoto maana ilikatika pesa na bill ya dollar mia mbili guess hapo nani amependeza zaidi mhh huyu dada mwenye black kapoteza!

ALIPOZI NA HAWA WAREMBO!

Mambo hayakuishia hapo pia alijichanganya na mafans kwa ajili ya picha na kadhalika....alipendeza kweli!

HEMEDY AKA PHD"MOVIE STAR!

Hii ilikua live show ya kukata na shoka hapa msanii mualikwa hemedy aka phd akingurumisha ndani ya ukumbi wa platinum hapa alionesha sio kama ni msanii wa playback peke ake ..nah aligonga live na topband...wape raha

Saturday, March 27, 2010

JAMANI TOPBAND TUNAWAZIMIA!

Moyoni kama vile namsemea huyu dada jinsi kazi inavomkuna sana kama namuona akitabasamu kama vile anatuambia jamani mnaimba vizuri mhh basi tabasamu lake hunifanya kuongeza nakshi zaidi kwenye show hizi za MASAI CLUB.

CHID MAPENZI!

Hapa namuona chid mapenzi aka designer akiwa amepozi na warembo wa TOPBAND wakishuhudia burudani ya nguvu bila ya kusahau kuwa mapenzi huwa anahusika kwa kiasi kikubwa kuchagua style ya nguo kwa ajili ya wanamuziki wa TOPBAND umeona!!

NYOMI!

Wananchi hawa hawakuwa nyuma kufatilia show kabambe toka kwa wakali TOPBAND kaka mwenye jezi alikua akifurahia kila nyimbo inayopigwa hebu cheki anavosmile halafu kama katokea kwa mzee KIBAKI!

SHE CANT BELIEVE!

Wakati naimba kibao cha ASHA huyu mrembo alishindwa kujizuia akaja moja kwa moja kwene stage na kuniangalia kwa ukaribu huo kama kweli naeimba ndo mimi kweli!mhh mambo ya masai club jamani yananoga!

Tuesday, March 23, 2010

CLUB AFRIQUE!

Its been 2 years since i had my last show in this east london based party club..yeah afta tha show i can remember gettin some supu,chapati and all kinda african dishes wow cant wait to face my friendly crowd....yeah LONDON MMEJIPANGA!

Monday, March 22, 2010

ANAITWA OMMY DIMPOZ.

Mimi hupenda kumuita sauti ya malavidavi huyu ndo dimpoz mkali wao,huwa hapendelei makuu anaipenda kazi yake na anahakikisha kila mstari anao back huwa kamili nways ukitaka kumjua vema njoo masai club au platinum...hapo ni jana akikamua na bendi yake platinum

KIFAA KIPYA!

Kama hujawahi kumsikia huyu dogo basi ninayo kila sababu ya kumnadi uweze kutambua kipaji chake yeye ni kati ya vijana wapya kujiunga na band hii lakini awezalo yeye huwafanya mashabiki kumpijia kelele za shangwe mhh anastahili kupewa nafasi zaidi aendeleze kipaji chake karibu sana TOPBAND.

BEAUTIFUL LADIES!

Warembo hawa walikuapo ndani ya nyumba PLATINUM jana wakishuhudia mambo ya TOPBAND kwa kweli walipendeza sana hadi tukaomba tuwapige picha mhhh hazikabi mwanzo mwisho!

Tuesday, March 16, 2010

Monday, March 15, 2010

AFTER THA SHOW IS AFTA THA PARTY!

Kutoka kushoto SAADA,REHEMA mama ya CHINA,MKALI,MARYAM na masaki hapo ni baada ya show kwisha mishale ya saa kumi unusu dah tulikua tukijadili wapi tukagonge misosi na viburudika..last minute tukadondoka MASAI CLUB kupiga mitori ya moto na chapati...wow!

HAPA HAWAINGII!

Ilipofika muda wake huyu dada aliamua kuwapoteza wenzake alipokikata kiuno vibaya sana haloo halooo mhh umeona mambo yetu haya jamani karibuni platinum kila jumapili!

NGOJA NIWAFUNIKE!

Ngoja na mie niwaoneshe hawa topband kama mtoto nimechezwa haiwezekani.......ana malele babu yao ana malele!

LADY KIDAWA!


Huyu anaitwa Lady Kidawa msanii wa TOPBAND hapa akiwaonyesha mfano wapenzi wa bendi yake....mhh umeona!

Sunday, March 14, 2010

NAE HAKUKUBALI!

hNae huyu aliyakata mauno vibaya sana unaona wenzako wanavokula raha na topband...mrembo huyu akusita alikwenda mpaka chini kisha akaanza kuinua mpaka juu!

HUO MTENDE!

Huyu mrembo aliamua kuukata mtende.........huo mtende wakati wa kukatika hukatika kati kati kaaaa!

DADA ZAKO!

Mambo ya masai club huwa si mchezo hawa warembo pia walishuhudia show ya kukata na shoka,karibuni jamani!

Wednesday, March 10, 2010

MAZOEZI KAMA MECHI!

Mazoezi ya leo hayakua madogo vijana walikamua sababu ya show nzito za week hii nahisi baadae itakua tamu sana pale masai club ujue kama kinondoni wamepata kiwanja chao cha kujidai na bendi nyao...karibu!

KOMAA KHALID...!

Well si kazi ndogo bt its an everyday job to keep my body in healthy condition so far am keepin this coz this coming week we are introducin tha NEW ERA" then hapo utaona why we been posted on TOP.

MAZOEZI MAKES PERFECT

Na baada ya kufanya show nzito huwa pia tunazukaga GYM na kama unavyoona ili niwe na stamina kabisa za kuwapa burudani ya kweli najifua kama hapo nikitengeneza mkono baaada ya kukimbia dakika 30 kwenye nashine...pia inasaidia kunipa pumzi zaidi napokua nadance huku nikipiga high PITCH...sasa ndo maana dada zako huwa hawakai chini!

SISI HAPA HAPA!

Wakina dada hawa kwa urembo wao na uhodari wa kuyakata mauno manager alishindwa kujizuia kuwapiga picha na wao hawakuwa na shobo walikua wakiserebuka maeneo ya kaunta tulivu huku wakipiga VYOMBO MH JAMANI MNAJUA KUCHEZA!

BRAZAMEN DULLY SYKES!

Brozamen dully sykes aka mtoto wa downtown hapa akifuatilia onesho la topband kwa makini sana huku akichezea iphone yake mhh kwa kweli alipendeza kweli na mtoko kama wa topband hebu angalia mastaa wa kweli na topband!

WANAONA GERE!

Eti wale wanaona gere"eyi wale wanaona gere" eeeeeh umeona eheee kiko wapi cha KUPAKA jamani hapao hapo unaziskia rap za topband huo ndo mpango hapo kati platinum unakosaje sunday hii!

Tuesday, March 9, 2010

UMEONA EEH!

Hapa ilikua inapigwa ule wimbo wa SIAMINI ndo ukaingia mduara huh haikua kawaida huyu dada alivokua akizungusha hadi akazawadiwa complimentary ya kuingia bendi yake free mwezi mzima hapo hapo mpaka chini mpaka chini"

MPANGO MZIMA!

Haya ndo mambo ya platinum huyu dada sikuwahi kumjua jina lake hebu ona alivochenguka na mziki wa bendi yake alifanya vitu adimu sana kiasi cha kutunzwa pesa nyingi hebu angalia hapo chini ya post hii!

Tuesday, March 2, 2010

WA KITAA!

WAkali wa TOPBAND wakiwa wanakula raha ndani ya ukumbi wa platinum jumapili hii.BABUU wa kitaa,MUBA mzazi na TITUS wakiangalia bendi yao ikitoa mziki wa kweli

MDUARA WA PLATINUM!

Mambo ya platinum hayo kina dada wakizungusha mduara haloo haloo...kama mwenyewe unavoona kwa raha zao!